Waathirika kushiriki katika utekelezaji wa Afua za ushawishi na utetezi, kutoa elimu ya TB katika jamii, kusimamia na kufanya tathmini ya mafanikio na changamoto za Kifua Kikuu katika jamii.
Tunapaza sauti moja ya jamii zilizoathiriwa na Kifua Kikuu kutoka maeneo na mazingira tofauti katika wilaya na mikoa yote ya Tanzania ili jamii ifurahie kwa kupata haki na uhuru katika huduma za afya.
Kuongeza ufanisi wa TTCN kama jukwaa la jamii zilizoathiriwa na Kifua Kikuu kwa kukusanya na kutoa taarifa sahihi za TB, kuwa na wanachama hai na wanaoshiriki katika ngazi zote kwenye jamii.